Thursday, April 26, 2012

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUCHAGUA MCHUMBA. Na Lazarus Mbilinyi.
Uchumba ni hatua ya kwanza ya kuwa mke au mume, hata hivyo ukichanganya mambo wakati wa uchumba inaweza kukupa soma ambalo utakuwa unajifunza maisha yako yote.

Yafuatayo ni mambo ya msingi sana kwa kijana ambaye ameokoka kuwa makini nayo.
Ieleweke kwamba kama hujaokoka unaweza kuyaona ni mambo ya kipuuzi hata hivyo kwa aliyeokoka ni uweza kwa ajili ya ndoa yake.

FAHAMU UMUHIMU WA KUFANYA MAAMUZI (decision)

Kuchagua mtu wa kuwa mke wako au mume wako ni uamuzi wa pili muhimu sana kwa maisha ya mtu duniani.Ulipookoka (receive salvation) uliingia katika mahusiano binafsi wewe na Mungu na unapooa au kuolewa unaingia katika mahusiano binafsi na mtu mwingine.Maana yake kuchagua mchumba ni uamuzi ambao si wa kukimbilia (rush) bila maombi na kufikiri kwa makini.

FAHAMU KUDUMU KWA UAMUAZI WA KUOA AU KUOLEWA (permanence)

Ulipoamua kuokoka maana yake ulikuwa ni uamuzi wa kudumu.Huwezi kuamua kuokoka leo na kesho ukaamua kurudi nyuma; ingawa wapo watu wa aina hiyo, ukweli ni kwamba true believers huendelea katika imani hata katika raha na shida.
      “I have decided to follow Jesus, no turning back, no turning back”

Ukishaoa au kuolewa hakuna kurudi nyuma, huwezi kuamka asubuhi na kusema
“ I have made a terrible mistake”
Au
“Nimeoa au kuolewa na wrong person” Sasa natafuta mwingine!
Hata kama umefanya makosa kuchagua mke au mume, usisahahu kwamba ndoa hudumu hadi kifo.Utawajibika kwa uzembe wako wa kuchagua mke au mume ovyo!

SHUKURU KWAMBA UMEOKOKA KABLA HUJAOA AU KUOLEWA

Kuwa umeokoka na upo single una opportunity kubwa sana ya kuwa na nice Christian marriage na Christian home kama kweli hizo ni ndoto zako.Huwa inasumbua sana kuishi na partner ambaye hajaokoka hasa kutokana na wewe kuokoka baada ya kuoa au kuolewa.Hivyo basi wewe ambaye umeokoka kabla ya kuoa au kuolewa unaweza kujenga foundation imara right from the start.

USIJARIBU KUWAZA KUFUNGWA NIRA NA ASIYEOKOKA
 (2Corith 6:14) Kuna watu wajinga wa maandiko huwa wanajifariji kwamba“Eti nikioana na mtu ambaye hajaokoka nitamshuhudia aokoke na nitamleta kanisani”.Imani ya Kikristo hairuhusu kuingiza watu katika imani kwa ahadi ya kuoana au kuolewa.

Maandiko tangu agano la kale husema wazi kwamba ambaye ameokoka hubadilishwa na ambaye hajaokoka.Au jiulize ukinunua gazeti chafu (mambo machafu) wakati unalisoma, wewe huwa unalitakasa gazeti au gazeti linakuchafua wewe na kuwa mchafu.Au je unaposikiliza miziki michafu, wewe huwa unaitakasa ile miziki au miziki ndiyo inakuchafua wewe?Acha uvivu wa kufikiri.

CHUNGUZA ZAIDI YA KUTAMKA KWAMBA YEYE NI MKRISTO (Ameokoka)

Si kila anayesema ameokoka ni kweli kwamba ameokoka au anaenda mbinguni wengine wanaenda manzese!.Angalia yule ambaye si anatamka tu kwamba ameokoka bali anayeishi maisha na matendo yanayoonesha kwamba kweli ameokoka.Kama anasema yeye ni apple tree mwambie akuoneshe apples zenyewe (fruits)
Angalia yule ambaye ni healthy believer.Uwe makini na yule ambaye bado ni mchanga sana kiroho na mpe muda zaidi (akue zaidi kwa muda unaotosha wewe kuamini kwamba ni kweli yupo serious na wokovu).Angalia yule ambaye ni stable anayependa Biblia na kanisa pamoja na ndugu waliokoka (wapendwa).Pia hakikisha vitu unavyoangalia na kwako ni kitu halisi.

ANGALIA YULE AMBAYE ANAPENDEZA AU MZURI

Hakikisha mtu unayetaka kuoana naye ni mzuri au anapendeza kwa ndani (beautiful on the inside).Uzuri wa ndani ni kitu ambacho ni thamani ya haki ya juu sana.Urembo na uzuri wa nje si issue sana, ukioa au kuolewa na mtu kwa sababu ya uzuri wa nje tu (good looks) itafika siku utakuwa katika total disappointment.
Je, miaka 30 ijayo pamoja na wrinkles usoni bado atakuvutia?
Je, ikitokea mke wako au mume wako akapata ajali ya uso wakati mpo kwenye ndoa akabaki amefunikwa na makovu meusi utaendelea kuvutiwa naye?
Ulioa au kuolewa na sura au na mtu?
Hakikisha unaoa au kuolewa kwa uzuri au kupendeza zaidi ya skin deep.Sijasema uoane na mtu ambaye ana sura kama chimpanzee, anyway hakuna mtu ambaye ana sura hiyo kwani mapenzi ni upofu!

USIWE NA HARAKA, SUBIRI
Miaka michache ya kusubiri ni kitu kidogo sana ukilinganisha na miaka 30, 40 au 50 ya kuishi pamoja katika ndoa.Kama miaka unayosubiri inakusaidia kuwa na maandilizi mazuri kwa ndoa yako basi hiyo ni baraka.Usichanganywe na watu wanavyoongea, hata kama rafiki zako wengi wanaolewa wewe msubiri Bwana.Wengine wamesubiri zaidi ya robo karne ili kuolewa na wakaolewa.
“A person can rush into marriage but cannot rush out of it”
JITUNZE WEWE MWENYEWE
Traditionally, bibi harusi huvaa gauni jeupe linalopendeza ambalo ni symbol kwamba amejitunza kimwili, kimaadili na kuwa ni bikira.Kabla ya ndoa unatakiwa kujitunza na kuwa mbali na uasherati.
Kuwa bikira lilikuwa jambo la msingi sana zamani za Biblia.(Mwanzo 24:16, Lk 1:27, 2:36)
Mungu bado anaona suala la kuwa bikira ni muhimu sana haijalishi wewe ni binti au ni kijana wa kiume.Wengi wameharibu ujana wao kwa kuambukizwa magonjwa ya zinaa kama vile UKIMWI nk na kujikuta ndoto za kuoa na kuolewa zinaota mabawa.

MFURAHIE BWANA (Kristo)
Kama kweli unataka kilicho bora kutoka kwa Bwana, na upo tayari kusubiri ukweli ni kwamba utapata au utakipokea.Zaburi 37:4, 84:11.Kama huna furaha wewe mwenyewe na Kristo, basi itakuwa ngumu sana kufurahia na mwingine yeyote mkiwa pamoja.

“When you can’t find peace and happiness within yourself, it’s useless to seek it elsewhere"

No comments:

Post a Comment