Tuesday, April 24, 2012

UFANISI WAKO KATIKA KUZITUMIA FURSA AMBAZO MUNGU ANAKUFUNGULIA HUTEGEMEA MAANDALIZI UNAYOFANYA KABLA YAKUJA KWA FURSA HIZO.


Mungu anapokufungulia Fursa yoyote ile anakusudia ifanyike msaada kwako katika kulitumikia kusudi lake. Na shetani ...anawinda Fursa hiyo hiyo ili akukwamishe na apitishe cha kwake ambacho kitakutoa kwenye makusudi ya Mungu.Kama hauna maandalizi ya kutosha kuhimili changamoto zinazoambatana na Fursa Mungu anazokufungulia ni dhahiri shetani atakupiga ngwala na utonufaika chochote na hizo Fursa. Labda niseme hivi, Maandalizi ni ya LAZIMA ili uweze kuzitumia vema Fursa mbalimbali Mungu atakazoachilia katika maisha yako.

Fikiri juu ya Kaini na Abeli walipopata Fursa ya kutoa sadaka mbele za Bwana.Ni wazi wote walikuwa na mda wa Maandalizi kabla ya kuitumia Fursa ile ya kutoa sadaka.Abeli alijiandaa sawasawa na muda wa kutoa ulipofika alitoa sadaka bora iliyogusa moyo wa Mungu naye akapata kibali.Lakini Kaini alizembea, hakufanya maandalizi ya kutosha na shetani alitumia udhaifu wake huo huo kumfanya asijiandae vizuri na ndio maana ulipofika mda wakutoa mbele za Bwana akatoa sadaka dhaifu ambayo haikupata kibali.
Shetani anajua kuna siri ya ajabu kwenye Fursa Mungu anazokufungulia na ndio maana anataka akupumbaze ili ujiandae kidhaifu kama Kaini.Nataka nikutie moyo mtu wa Mungu,haijalishi unapitia hali gani katika maisha yako,unapaswa kufahamu hili,zipo Fursa Mungu anaenda kuachilia maishani mwako ili kukutoa mahali ulipo na kukupeleka pale anapokukusudia.Fanya maandalizi yakutosha ili uweze kabiliana na changamoto utakazo kutana nazo wakati Fursa hizo zitakapo funguliwa.

Zifuatazo ni njia kadhaa ambazo zitakusaidia kujiandaa kukabiliana na changamoto zinazokuja mbele yako ili uzitumie vizuri Fursa Mungu atakazo kufungulia;

•Kwa kuwa na malengo. Mithali 29:18.
•Kwa kuomba bila kukata tamaa (ombeni msije mkaingia majaribuni).
•Tafuta kujua kusudi la Mungu katika maisha yako i.e kwa nini uliumbwa. Ukijua kusudi ni rahisi pia kujua mipango yake katika maisha yako.
•Ukishajua nini wajibu wako hapa duniani, basi tekeleza kwa bidii, moyo na uvumilivu hayo majukumu. Ongeza ufahamu katika nyanja (field) yako ili upate maarifa ya kukusaidia uwe na ufanisi mzuri zaidi.
•Kuwa makini na maisha yako (Zaburi 1:1). Hili litakujengea maisha ya nidhamu ili kuhakikisha unakaa kwenye mpango wa Mungu. Kuishi katika mpango wa Mungu kuna gharama zake. Gharama kubwa ni kujikana, ni lazima ujifunze na ukubali kuyahesabu mambo mengine kuwa hasara ili shauri la Kristo liweze kufanikiwa.
•Weka ndani yako/tafakari neno/sheria ya Bwana usiku na mchana. Hii itakupa kuona njia ikupasayo kuiendea. “Neno la Bwana ni taa ya miguu yangu”.
•Jifunze kuwa na muda wa utulivu wa kuomba na kuwaza. Mungu huwa anasema katika utulivu. Utulivu wako ni fursa kwa Mungu kukufunulia FURSA za kukabiliana na changamoto unazozipitia na zinazokuja.
Mungu akubariki, naamini ukiyaweka haya katika utendaji taratibu utaanza kuona fursa ambazo Mungu anazileta kwako ili kukufanikisha. Kumbuka siku zote kwamba mawazo yake ni ya amani, kukupa tumanini siku zako za mwisho.Shaloom!!!!

No comments:

Post a Comment