Thursday, July 5, 2012

“USIJARIBU KUITAMANI KANANI KAMA HAUKOTAYARI KUPAMBANA NA MAJITU (CHANGAMOTO)”

Ni Kweli Kanani Kuna Maziwa Na Asali,Tena Ni Nchi Nzuri Ajabu, Lakini Kuna Majitu (Changamoto) Yanayoishi Humo.Na Hivyo Yeyote Anayetaka Kufurahia Mazuri Hayo Y...a Kanani Ni Lazima Awetayari Kukabiliana Na Majitu(Changamoto) Ndani Ya Hiyo Kanani.Kama Unayaogopa Majitu(Changamoto) Sahau Habari Za Maziwa Na Asali Maana Hutoyapata.

Umewahi Kujiuliza Kwanini Mungu Akuandalie Kanani Yenye Maziwa Na Asali Na Wakati Huo Huo Aruhusu Majitu Yakae Ndani Ya Hiyo Kanani? Kwanini Mungu Asiwaondoe Majitu Hayo (Changamoto Hizo) Kwanza Na Ndipo Akuruhusu Uimiliki Kanani Hiyo? Hii Ni Siri Ya Ajabu Mtu Wa Mungu Na Unapaswa Ufahamu. “Katikati Ya Majitu (Changamoto) Kuna Maziwa Na Asali Na Hakuna Jinsi Ya Kuyafurahia Mazuri Hayo Bila Ya Kuyakabiliana na Majitu (Changamoto)”. Na Ukiona Majitu Yanaongezeka Jua Kuna Shehena Ya Maziwa Na Asali Kubwa Kuliko Kawaida Hapo Mahala. Ukijaribu Kuyakimbia Majitu (Changamoto) Jua Ndo Unaikimbia Kanani Yako Na Vyote Vizuri Vilivyomo Ndani Yake.

Pengine Umeikaribia Kanani Yako Mara Nyingi Lakini Kwasababu Umeyaona Majitu (Changamoto) Ukaogopa Na Umeamua Kurudi Nyuma.Ni Heri Ukalijua Hili Mtu Wa Mungu,Hakuna Jinsi Utakayo Weza Kufaidi Mazuri Ya Kanani Kama Hutaki Kuyakabili Majitu(Changamoto) Yaliyomo Ndani Ya Hiyo Kanani.Ukisoma Habari Ya Wapelelezi Kumi Na Wawili Kwenye Kitabu Cha Hesabu Sura 13 & 14, Maandiko Yanatuambia Ni Wale Tu Walionyesha Uhodari Na Utayari Wakutaka Kuyakabili (Majitu) Changamoto (Kalebu Na Yoshua) Ndio Waliopata Kibali Cha Kuiingia Nchi Ya Ahadi(Kanani).
Ukiamua Kuogopa Kuyakabili Majitu Na Kuyaachia Ya Faidi Maziwa Na Asali Ndani Ya Kanani Mungu AliyoKukusudia, Uamuzi Ni Wako.Ukiamua Kuyakabili Majitu Ili Umiliki Na Kuyafurahia Mazuri Ya Kanani Yako.Uamuzi Ni Wako.Chagua Lako!Shaloom!

“Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu” <<Zaburi 23:5a>>


No comments:

Post a Comment