Sunday, July 29, 2012

“KUOKOKA PASIPO KUTEMBEA KWENYE KUSUDI LA MUNGU HAKUMTISHI SHETANI”

Shetani Haogopi Watu Waliookoka, Anaogopa Watu Waliookoka Na Wanaotembea Kwenye Makusudi Ya Mungu. Vita Ya Shetani Si Kukuzuia Wewe Kwenda Mbinguni Tu, Bali Ni Pamoja Na K...uhakikisha Kwamba Makusudi Ya Mungu Humu Duniani Hayafanikiwi.Na Ndio Maana Wakati Mwingine Anaweza Asilete Upinzani Kwenye Kuokoka Kwako.Akakuacha Uokoke Bila Upinzani Wowote, Lakini Mara Tu Baada Ya Kuokoka Akakupiga Vita Na Kukutengenezea Mazingira Ya Kukufanya Uishi Nje Ya Kusudi Mungu Alilonalo Juu Ya Maisha Yako.

Kwenda Mbingu Wakati Umetumia Maisha Yako Nje Ya Makusudi Ya Mungu Ni Kuutia Hasara Ufalme Wa Mbinguni.Mungu Amekuokoa Sio Tu Uende Mbinguni, Bali Pia Uishi Maisha Ya Ushindi Huku Ukilitumikia Kusudi Lake Hapa Duniani.Ndio Maana Kuna Maelfu Ya Watu Wameokoka Na Shetani Amekua Akiwavuruga Kila Eneo Kwasababu Hawatembei Kwenye Kusudi Mungu Alilowaitia. Kamwe Usitegemee Masaada Wa Mungu Nje Ya Kusudi. Na Ukikaa Nje Ya Kusudi Ujue Unampa Shetani Uhalali Wa Kukuvuruga, Na Mungu Hawezi Kukutetea Nje Ya Kusudi.Ndio Maana Ni Muhimu Ujue Hili, Ukiokoka Na Hautembei Kwenye Makusudi Ya Mungu Jua Hauna Madhara Kwa Shetani.Shalooom!

Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa;<< Yeremia 1:5a>>

No comments:

Post a Comment