Monday, October 8, 2012

"MWENYE MAONO HUWA SELECTIVE, HAOI/HAOLEWI KWASABABU TU KUNA MTU AMEONYESHA NIA"

Haijalishi Una Njaa Ya Kuolewa/Kuoa Kiasi Gani, Kama Umebeba Maono Ya Kimungu Ndani Yako, Chunga Sana Maamuzi Yako Juu Ya Nani Unaunganisha Naye Maisha Yako Kama Mume Au Mke.Kumbuka Si Kila Anayekuja Kwako Kwa Lengo La Kukuoa/Kuoa Anamsukumo Wa Kimungu Ndani Yake.Wengine Wanakuja Kwako Kwa Hila, Na Shetani Anataka Kuwatumia Kuua Maono Mungu Aliyoweka Ndani Yako.Laiti Samsoni Angelijua Hila Iliyokuwa Ndani Ya Moyo Wa Delila Dhidi Ya Kile Mungu Alichoweka Ndani Yake, Kamwe Asinge Thubutu Kujenga Hata Ukaribu Naye.

Hupaswi Kulisha Njaa Yako,Lisha Maono Mungu Aliyoweka Ndani Yako.Wengi Wamejikuta Wakilisha Njaa Zao Za Kutaka Kuwa Na Wenza Na Si Maono Yao, Na Hivyo Kujikuta Wakioa/Kuolewa Na Watu Ambao Ni Waua...
Maono (Vison Killer). Haijalishi Umengoja Kwa Muda Mrefu Kiasi Gani Au Umri Wako Unakimbia Kiasi Gani, Chunga Sana Maamuzi Yako Usije Ukakuta Unalisha Njaa Yako Na Kuunganisha Maisha Yako Na Mtu Yeyote Tu Maadamu Ametokea.

Maono Mungu Aliyoweka Ndani Yako Yana Thamani Kuliko Unavyofikiri.Kumbuka Njaa Haichagui,Njaa Ilimfanya Esau Asione Thamani Ya Uzaliwa Wake Wa Kwanza Na Hivyo Kupoteza Baraka Zote Zailizobebwa Ndani Ya Ile Nafasi.Njaa Yako Ya Kuolewa/Kuoa Isije Kufanya Ukapoteza Maono Yenye Thamani Ambayo Mungu Ameyaachilia Moyoni Mwako. Kaa Na Mungu Vizuri Yeye Anamjua Mwenza Sahihi Kwa Ajili Yako,Tena Atakaye Kusaidia Kukamilisha Maono Yaliyo Ndani Yako.Shaloom!

No comments:

Post a Comment