Sunday, July 29, 2012

“UMEKUJA DUNIANI KWASABABU UNAHITAJIKA”
Mshukuru Mungu Kwasababu Wakati Unazaliwa Changamoto Ndani Ya Dunia Hii Zilikuwa Hazijaisha, Vingenenyo Ungekuwa Hauna Kazi Ya Kufanya Hapa Duniani.Tena Usijeukafikiri Ni Bahati Mbaya Kwamba Umezaliw...a Ndani Ya Nchi/Familia Yenye Changamoto Chungu Mzima Na Ukaanza Kujichukia Na Kulaani. Nataka Ufahamu Hili Mtu Wa Mungu, “Wewe Ni Original (Sio Fotokopi) Na Umekuja Duniani Kwasababu Unahitajika”

Mungu Amekuleta Duniani Kama “Spana” Maalumu Kwa Ajili Ya Kukutumia Kufungulia Nati (Changamoto) Zote Zilizogoma Kufunguka Katika Mazingira Yako. Amekudesign Katika Ufanisi Wa Kipekee Kiasi Kwamba Hakuna Nati Aliyoikusudia Aifungue Kwakukutumia Wewe Ambayo Itakayogoma Kufunguka Ikiwa Utakubali Akutumie. Kuna Nati (Changamoto) Chungu Mzima Hazija Funguka Mpaka Leo Hii Katika Familia Yako,Katika Nchi Yako Kwasababu Tu Umekataa Kukaa Kwenye Nafasi Yako Ili Mungu Akutumie Kuzifungua Nati (Changamoto) Hizo.

Ndio Maana Nataka Nikukumbushe Hili Leo, “Umekuja Duniani Kwasababu Unahitajika”.Mungu Anakuhitaji,Jamii Inakuitaji,Kanisa Linakuhitaji,Familia Yako Inakuitaji.Usipo Simama Kwenye Nafsi Yako Sawasawa,Kuna Nati(Changamoto) Humu Duniani Hazita Funguka Maana Wewe Ndiye Uliyedesigniwa Na Mungu Akutumie Kushughulikia Hizo Nati(Changamoto).Simama Katika Nafasi Yako Mtu Wa Mungu Maana Saa Ya Wokovu Ni Sasa.Shaloom!

No comments:

Post a Comment