Wednesday, May 9, 2012

YUPO MUNGU ANAYESHUGHULIKA NA MAMBO YAKO

Nasema yupo Mungu anayeweza kuugeuza uteka wako na kuibadili historia ya maisha yako rafiki yangu.Haijalishi unapitia katika mapito ya namna gani, au umeteseka kwa muda mrefu kiasi gani.Ninayo habari njema kwako, Yuko Mungu anayeshughulika na Mambo yako.

Biblia inasema,
“Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishugulisha sana na mambo yenu”. <<1 Petro 5:7>>.
...
Inawezekana ni haja za moyo wako zinakufanya ukose amani na ufikiri hakuna tena jibu au msaada wa kukuvusha kutoka mahali ulipo.Sikiliza mtu wa Mungu, haijalishi unapitia katika shida kubwa kiasi gani mpaka unafika mahali unafikiri ulimwengu mzima umekusaliti.Kamwe usije ukasahau jambo hili, yupo Mungu anayeshughulika na maisha yako na hawezi kukuacha kamwe.

Yeye ni mwaminifu tena anashika maagano,na ahadi zake ni kweli na amina.Yeye anapigana upande wako, usikubali kukatishwa tamaa na mazingira au hali yeyote unayopitia.Yeye yuko tayari kubeba fadhaa zako badala yako.Mtwike yeye fadhaa zako, mtwike yeye maumivu yako,mtwike yeye magumu yako, mtwike yeye haja za moyo wako, maana yeye hushughulika na mambo yako. Shaloom!

No comments:

Post a Comment