Sunday, July 29, 2012

USIJARIBU KULEGEZA MSULI WAKO WA IMANI KAMA UNAJUA HUJAIINGIA KANANI YAKO

Ni Muhimu Kukumbuka Hili, ‘‘Unapo Piga Hatua Moja Mbele Kwenye Eneo Lolote La Maisha Yako Iwe La Kiroho,Kibiashara,Kielimu,Au Kwenye Lolote Lile Linalombariki Mungu....Kamwe Usije Ukajisahau Na Kulegeza Msuli Wako Wa Imani.’’ Shetani Hatokubali Kamwe Uiendee Hatima Yako Na Hivyo Atakufuatilia Kwa Namna Yeyote Ile Ili Akurudishe Nyuma(Utumwani).

Na Moja Ya Kitu Atakacho Pambana Kukiharibu Ni Imani Iliyojengeka Ndani Yako.Anajua Akibomoa Imani Iliyojengeka Ndani Yako, Utaanza Kuangalia Ukubwa Wa Bahari Iliyo mbele Yako,Utaanza Kulihofu Jeshi Linalo Kufuatailia Nyuma Ili Kukurudisha Misri.Tena Utasahau Ukuu Na Uaminifu Wa Mungu Aliyekufikisha Mahali Ulipo. Na Mwisho Atakurejesha Nyuma (Utumwani) Kirahisi Kabisa.

Kadiri Unapotoka Utukufu Kwenda Utukufu Ndivyo Adui Anavyozidi Kujipanga Na Kuongeza Jitihada Katika Kukufuatilia.Uimara Wa Imani Yako Ndio Utakao Kusaidia Kupata Msaada Wa Mungu Pale Unapokutana Na Upinzani. Kumbuka,Mungu Hakukutoa Misri Ili Urejee Tena Huko,Wala Hakukutoa Misri Ili Uje Kuangamia Njiani. Na Ndio Maana Kama Unajua Umepiga Hatua Fulani Lakini Haujaifikia Kanani Yako Usije Ukajaribu Kulegeza Msuli Wako Wa Imani.Kumbuka Bado Utahitaji Msaada Wa Mungu Ili Uifikie Kanani Yako, Na Pasipo Imani Iliyojengwa Sawasawa Itakuwa Ni Vigumu Kupokea Msaada Huo Na Hata Kuzikabili Changamoto Zitakazokujia Mbele Yako.Shaloom!


‘Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu’.<<Waefeso 6:15 >>
See More

No comments:

Post a Comment