Monday, September 3, 2012

‘’UNAHITAJI UFUNUO MPYA UTAKAOACHILIA MBINU MPYA ILI UZIKABILI CHANGAMOTO MPYA KATIKA KILA UTUKUFU MPYA MUNGU ANAOKUPELEKA‘’

Kufaulu Kwako Katika Kuzikabili Changamoto Za Jana Hakukupi Garantii Ya Kwamba Utafaulu Kwenye Kukabiliana Na Cha...
ngamoto Unazokutana Nazo Leo Au Utakazo Kutana Nazo Kesho.Ndio Maana Usijaribu Kuingia Katika Kiwango Kipya Kwenye Eneo Lolote La Maisha Yako Ukiwa Na Mbinu Za Zamani Pekee Na Ukategemea Kufaulu Vizuri Katika Kukabiliana Na Changamoto Utakazokumbana Nazo Kwenye Hicho Kiwango Mungu Atakacho Kupeleka.

Kumbuka Kadiri Mungu Anavyokutoa Kwenye Kiwango Kimoja Cha Utukufu Kwenda Kwenye Utukufu Mwingine Ndivyo Adui Anavyozidi Kujipanga Na Kuongeza Jitihada Katika Kukufuatilia Na Kukupinga.Upinzani Uliokutana Nao Kwenye Utukufu Mungu Aliokupitisha Jana Nitofauti
Kabisa Na Upinzani Utakao Kutana Nao Kwenye Utukufu Mungu Anaokupitisha Leo Au Kesho.Ndio Maana Mbinu Ulizozitumia Kukabiliana Na Changamoto Za Jana Zinaweza Zisiwe Bora Leo Kama Itaibuka Changamoto Mpya Isiyofanana Na Ile Uliyokabiliana Nayo Jana.

Daudi Alijua Hili Na Ndio Maana Alikataa Mavazi Na Dhana Za Kijeshi Alizotaka Kuvalishwa Na Mfalme Sauli Wakati Anajiandaa Kumkabili Goliath. Daudi Alijua Mapema Kwamba Hivyo Vitu Vya Sauli Ni Mbinu Za Zamani Na Hazina Msaada Vinginevyo Jeshi La Israel Lisingeshindwa Kumkabili Goliathi Hapo Kabla.Alijua Anahitaji Ufunuo Mpya Toka Kwa Mungu Na Si Ule Wa Zamani Wa Mfalme Sauli.Ni Ufunuo Mpya Ulioachilia Mbinu Mpya Na Ndizo Zilizomvusha Daudi Dhidi Ya Goliathi.

Maombi Yangu Na Dua Yangu,Ni Mungu Akakupe Ufunuo Mpya Utakao Achilia Mbinu Mpya Za Kukabiliana Na Changamoto Mpya Utakazokutana Nazo Kadiri Anavyozidi Kukupeleka Kwenye Utukufu Mpya Kila Inapoitwa Leo.Shaloom!!

No comments:

Post a Comment