Friday, March 30, 2012


KAMA UNATAMANI KUTAFSIRI NDOTO YA MFALME,KAMWE USIPUUZE KUTAFSIRI NDOTO YA MFUNGWA


 

Kabla ya kuitwa kuitafsiri Ndoto ya Mfalme (Pharao), ilimpasa YUSUFU kujenga msuli kwa kutafsiri ndoto ndogo ndogo za wafungwa wenzake... mule Gerezani. Uaminifu na Ufanisi wa Yusufu katika kufanyia kazi Fursa Ndogo Ndogo (Limited Opportunities) zilizotokea mule Gerezani ndicho kilichomfanya akumbukwe na kupewa FURSA KUBWA zaidi yakutafsiri Ndoto ya Mfalme (Pharao).

Hata DAUDI hakudharau Fursa ya kupambana na Dubu kule PORINI alipokuwa anachunga kondoo.Ilipokuja FURSA ya Kupambana na GOLIATH wakati Jeshi lote la Israel likiwa limerudi nyuma na kuogopa, msuli wa DAUDI ulikuwa umekaa sawasawa kwa ajili ya kupambana. Israel walikuwa wakimwona GOLIATH kama tatizo kubwa (A VERY BIG PROBLEM),Lakini Daudi alikuwa akimwona GOLIATH kama Fursa kubwa (A VERY BIG OPPORTUNITY). Na Mungu alitumia fursa hiyohiyo kumpeleka Daudi kwenye Kiwango cha juu zaidi.

Sijui unapita katika changamoto gani za kimaisha,au unakutana na upinzani kwa kiasi gani kwenye mazingira yako, yawezekana uko GEREZANI kama Yusufu au umesahauliwa PORINI kama Daudi, uwe na uhakika zipo fursa ndogo ndogo Mungu ataachilia ili kukuandaa kwa ajili ya kukupeleka kwenye kiwango kizuri zaidi katika maisha yako.Fanya utafiti kwenye mazingira yako, zipo FURSA, yawezekana unaziona NDOGO na kuzidharau,lakini uwe na uhakika, UAMINIFU wako katika kutumia FURSA hizo ndogo,unamaana sana machoni pa Mungu katika kukufungulia Fursa zilizo BORA zaidi.

No comments:

Post a Comment