Friday, March 30, 2012

FURSA YOYOTE MUNGU ANAYOKUFUNGULIA IMEFUNGWA NDANI YA MUDA 

Ni vema ukajua, Fursa yoyote ile ambayo Mungu ataiachilia katika maisha yako imefungwa ndani ya Muda.Ukicheza na muda uliobeba hiyo Fursa uwe na uhakika utakuwa... umecheza na Fursa iliyobebwa ndani ya huo muda.
Yapo mazingira Mungu ataachilia Fursa katika maisha yako ili kukupeleka kwenye hatua nyingine au kukuvusha kutoka mahali ulipo.Lakini haijalishi ni Fursa kuu kiasi gani, ili ikuletee matunda yaliyo kusudiwa itategemea jinsi gani utakavyo uheshimu Muda uliobeba hiyo Fursa.

Unayakumbuka maneno haya? “Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako” << Luka 23:42>>
Haya ni maneno ya mhalifu mmoja kati ya wale wahalifu wawili waliosulubiwa pamoja na Yesu pale msalabani.Ni dhahiri, yule mhalifu hakuwa na jinsi yeyote ya kuiokoa roho yake, maana alijua kifo kilikuwa kinamkabili.Lakini kwa neema, katikati ya mazingira yaleyale ya msalabani, Mungu aliachilia FURSA ya kuokoa roho yake. Hakukuwa na muda mwingine,ile Fursa ili achiliwa ndani ya dakika zile zile chache tu, na maamuzi yake ndani ya mda ule ndiyo yaliyoamua hatima ya roho yake baada ya pale msalabani.
Fikiri nini ingekuwa hatima ya yule mhalifu kama angecheza na zile dakika chache alizozitumia kujutia na kutubia uovu wake pale msalabani? Ni Fursa pekee ambayo Mungu aliyoiachilia, na kama asingeitumia vizuri ndani ya muda husika ni dhahiri hatima yake ingekuwa ni mbaya kuliko unavyodhani, maana angekufa katika dhambi na maandiko yanatuambia mshahara wa dhambi ni mauti. 

Yawezekana Fursa za namna kama hii Mungu amekuwa akiziachilia katika maisha yako na hukujua thamani ya muda unaobeba Fursa hizo.Labda ni wapendwa wamekuwa wakikushuhudia kwa habari ya kuyatoa maisha yako kwa Yesu na wewe umekuwa ukidharau,ukihairisha kila siku na kuchezea Muda uliobeba hiyo Fursa.Maadamu Fursa hiyo imefungwa ndani ya mda,nataka utambue kwamba ukicheza na huo muda,unacheza na hiyo Fursa pia.
Ni huzuni na ni hasara kiasi gani kudumu katika dhambi wakati FURSA ya kukutoa katika hila jalala imeshaachiliwa maishani mwako.Yule Mhalifu alijua thamani ya Muda uliyobeba FURSA ya yeye kuutubia uovu wake.Alijua hana mda wakuchezea tena,hakujua nini itakuwa hatima ya Roho yake baada ya pale msalabani na ndio maana aliamua kudandia gari ya Yesu na kufanya uamuzi wa busara ndani ya zile dakika chache na ndicho kitu pekee kilichookoa roho yake.

 Katika 2wakorinto 6:2 maandiko yanatuambia SAA YA WOKOVU NI SASA (muda wa kuyatoa maisha yako kwa Yesu ni sasa).Fursa hii imeachiliwa na imefungwa ndani ya muda, fanya uamuzi wa busara kama yule mhalifu maana Muda ulioachiliwa ukipita uwe na uhakika na Fursa iliyoachiliwa itapita. Kamwe usicheze na Muda uliobeba FURSA ya wewe kuyatoa maisha yako kwa Yesu, kumbuka wakati uliokubalika ni sasa na SAA YA WOKOVU NI SASA.Shaloom.
Prepared by
MASSAWE GILBERT
SAA YA WOKOVU NI SASA

I Like this quote I dislike this quote  “Success always comes when preparation meets opportunity” Henry Hartman

No comments:

Post a Comment