Friday, March 30, 2012

MUNGU HAWEZI AKAACHILIA WAZO LA BIASHARA NDANI YA MOYO WAKO ALAFU ASIKUFUNGULIE MLANGO WA KUPATA MTAJI.



Mungu anapoachilia wazo ndani ya moyo wa mtu iwe la biashara au la jambo lolote, uwe na uhakika, kwa jinsi ya rohoni hilo wazo ameshal...itazama hadi mwisho wake i.e kiutekelezaji na matokeo yake.
Ni vizuri ufahamu hii mistari itakusaidia, maana utakujengea msingi mzuri wa kulielewa wazo la Mungu anapoliachiliwa ndani moyo yako.
<<Isaya.46:9-10>> inasema,“Kumbukeni mambo ya zamani za kale maana mimi ni Mungu wala hapana mwingine, mimi ni Mungu wala hapana aliye kama mimi. Nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado, nikisema, shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote”.

Kwa lugha nyingine anakuambia ya kwamba, hiyo biashara unayotaka kuifanya, kabla sijaweka wazo langu ndani ya moyo wako, nilipita kwa jinsi ya rohoni nikalitekeleza na nikafika mpaka mwisho, nikaona matokeo yake yatakuaje na ndipo nikaliachilia hilo wazo ndani ya moyo wako ili ulidhihirishe kwa jinsi ya mwilini.

Mungu akiachilia wazo na ukalielewa ndani ya moyo wako uwe na uhakika atakufungulia milango maana ni lazima litaufikia mwisho wake.Utashangaa atakupa kibali mahali ambapo hukutegemea, atakukutanisha na watu ambao hata ujawahi fikiria kukutana nao, utashangaa milango itakavyofunguka mpaka hilo wazo litakapo fanyika mwili.Fikiri Yusufu hakuwa raia wa misri lakini angalia jinsi alivyopata kibali na kuwa waziri mkuu hukohuko ugenini. 



 Kama Mungu ameachilia wazo la kibiashara ndani ya moyo wako usikatishwe tamaa na mazingira,uwe na uhakika litafanyaka mwili na kufika kwenye kiwango kilicho kusudiwa.Yusufu alikuwa na ndoto(wazo) ndani yake, na ilipojulikana upinzani uliinuka, alipitia mengi mpaka kuifikia ile ndoto yake.Kuna mahali ilimlazimu kuchukiwa hata na ndugu zake, aliuzwa kama mtumwa, alifungwa gerezani bila hatia.Lakini haya yalikuwa ni mapito na changamoto tu,hayakuweza kuua ndoto au wazo ambalo Mungu alikuwa ameliachilia ndani ya moyo wake.


  Amua kumshirikisha Mungu katika mambo yako ili aachilie vya kwake ndani yako ambavyo vitakufanikisha na kukufikisha mahali anapokukusudia.SHALOOM

No comments:

Post a Comment