Wednesday, May 9, 2012

JENGA NIDHAMU KATIKA KUTUMIA FURSA MUNGU ANAZOKUFUNGULIA ILI ZIKUNUFAISHE

Mungu hakukuumba kwa lengo la kuijaza dunia tu. Umekuja duniani kwa kusudi lake maalum. Hivyo ili kuhakikisha kusudi lake linafanikiwa Mungu hutengeneza mazingira ya kuhakikisha kusudi lake kupitia wewe linafanikiwa. Mkakati mmoja wa hayo mazingira ni kukuletea fursa za wewe kuokoka, kusoma, kuoa/kuolewa, madaraka, uongozi, fedha, muda, vipawa au vipaji mbalimbali nk. Si watu wengi leo wanaojua namna ya kutumia fursa hizo kwa faida ya ufalme wa Mungu.

Usije ukadhani utajiri, elimu, au madaraka uliyonayo ni kutokana na nguvu zako au wazazi wako au kwa kuwa mna asili ya utajiri. Je, umeshawahi kujiuliza kwa nini wewe uwe hivyo na si mwingine awe kama wewe. Siri ni hii, ipo sababu ya Mungu kukupa vyote ulivyo navyo s...asa, kama fursa/nafasi ya kukamilisha kusudi lake hapa duniani kupitia wewe. Unapaswa kuishi na kuyakabidhi maisha yako kwa Bwana kwa mfumo ambao atakuwa tayari kukutumia wewe kupitia fursa alizokupa kwa wakati atakao yeye na si wewe ili kufanikisha kusudi lake.

Huwezi kufikia kiwango cha juu cha mafanikio yako kiroho na kimwili kama hautajua au kuwa na nidhamu ya kutumia vema fursa zote ambazo Mungu anakupa maishani mwako. Kumbuka kwamba fursa ni nafasi inayojitokeza kama mlango/njia ya wewe au wengine kupita kutoka kwenye eneo ambalo ulikuwa umekwama na pia ni nafasi inayokuja kukuonyesha mlango wa kupita siku utakapokuwa kwenye eneo ambalo huna msaada.
 

No comments:

Post a Comment