Thursday, May 10, 2012


JINSI UNAVYO LITAZAMA TATIZO NDIO TATIZO


 Umewahi kujiuliza kwanini kuna mambo ambayo kwako yanaonekana kuwa ni misiba, shida, vikwazo, mitihani, au magumu, lakini kuna watu katika mazingira yako hayo hayo na matatizo hayo hayo wao wanayaon...a kama ni fursa au rasilimali tosha za kuwapeleka kwenye hatua nzuri zaidi ya kimaisha? Kwanini pale ambapo panaonekana pana mashimo au ukuta kwako, wengine wanaona madaraja au ngazi za kwasaidia kuelekea kwenye kiwango bora zaidi cha kimaisha?

Fikiri kilichotokea wakati Jeshi la Israel lina pambana na Goliath. Jeshi la Israel lilimwona Goliath kama tatizo kubwa (a very big problem) na hii ilitengeneza hofu ndani yao wakajikuta wana mwogopa na wakaamua kurudi nyuma.Lakini katika mazingira hayo hayo Daudi aliposikia habari ya Goliath, ndani yake kulikuwa na ujasiri watofauti, alikuwa na kiu ya kupambana na Goliath ambaye Jeshi kubwa la Israel lilikuwa likimwogopa.Yeye alimwona Goliathi kama fursa kuu (a very big target). Tena aliona ndio nafasi pekee yakumpeleka kwenye ukuu Mungu aliomkusudia. Na hili lilimpa ujasiri wakumwendea na kupigana naye.

Ngoja ni kupe siri mtu wa Mungu, “Mshukuru Mungu kwasababu wakati ulipozaliwa changamoto za kimaisha zilikuwa hazijaisha, vingenenyo ungekuwa hauna kazi ya kufanya hapa duniani.Umekuja duniani kwasababu unahitajika tena kwa ajili ya special assignment. Mungu amekuleta ili akutumie kwa ajili ya kuleta majibu juu ya changamoto zinazo kuzunguka au zinazoikabili jamii yako.Lakini itategemea jinsi unavyo zitazama changamoto hizo.Jinsi unavyo itazama changamoto ndio changamoto yenyewe.

Ukiona Goliath ameinuka katika mazingira yako au katika jamii yako, uwe na uhakika Yupo Daudi ambaye Mungu amemwandaa kwa ajili ya kumkabili Goliath huyo(changamoto hiyo).Mungu anamngoja Daudi wa eneo hilo akae katika nafasi yake sawasawa na aitazame changamoto hiyo kwa jinsi yeye Mungu anavyo itazama ili amtumie kumpiga huyo Goliath(kuikabili hiyo changamoto).Na ndio maana kama umeokoka na katika mazingira mnakabiliana na changamoto yoyote uwe na uhakika wewe ndiwe Daudi wa hilo eneo ambaye Mungu anataka ukae kwenye nafasi yako hili akutumie kuleta majibu ya changamoto hizo.
Na ndio maana bibilia inatuambia katika <<Warumi 12:2 >>

"Wala msifuatishe namna ya dunia hii bali geuzwe kwa kufanywa upya nia zenu mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza na ukamilifu."

Watu wadunia wanajinsi yao ya kutazama changamoto, wana mitazamo yao juu ya changamoto, wana fikra na nia zao juu ya changamoto, maandiko yanatuambia, tusifuatishe namna watu wa dunia wanavyoenenda.Hii ina maana watu wa mataifa wana jinsi yao au utaratibu wao wa kutazama changamoto, au wa kuzikabili changamoto.Lakini sisi baada ya kumjua Mungu wetu, tunapaswa tugeuzwe na kufanywa upya nia zetu, fikra zetu, mitazamo yetu, kuenenda kwetu.

Jinsi unavyotazama changamoto unazo kabiliana nazo ndio tatizo mtu wa MunguUkitazama kama watu wadunia wanavyo tazama utaona tatizo kubwa, lakini ukitazama kwa jicho la kimungu (kwa imani iliyojengwa juu ya neon la Mungu.Utashangaa changamoto zinageuka fursa za kukupelka mahali Mungu anapokukusudia

Maombi yangu na dua yangu ni kama vile Mtume Paulo alipokuwa akiwaombea waefeso. <<Waefeso1:17-22>>

“Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye.Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake; aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote."

No comments:

Post a Comment