Wednesday, June 27, 2012

NIPE CHANGAMOTO, NIPE MATATIZO NAMI NITAKUONYESHA IMANI YANGU

Ukitaka kujua imani Ya Mtu ikoje au inafanya kazi kiasi gani,Mtazame wakati wa matatizo au Changamoto zinapo mkabili. Hapo ndipo utajua kama huyu ana imani ya kweli katika Kri...sto au anabipbip tu kama msindikizaji.

Mara nyingi Changamoto zinapotokea hapo ndipo unapoweza kufahamu imani za watu zimejengwa wapi na zinafanya kazi kwa jinsi gani.Hapo ndipo utawaona wa Kwenda kwa waganga,utawaona wa wakukata tamaa,utawaona wakujinyonga,wakuanza kumtafuta mchawi,wakunyoosheana vidole,humohumo kwenye changamoto utawaona watakakao ng'ang'ana na Yehova ili wapate majibu yao.

Siku zote imani ujidhihirisha panapo tatizo au changamoto.Wakati mambo yanaenda vizuri imani ya mtu huwa ni vigumu kidogo kujua ina nguvu,au ni dhaifu kiasi gani au ni kubwa kiasi gani.Ngoja Changamoto zitokee Ndipo utajua Huyu mtu ana imani na inafanya kazi kwa kiasi gani.

Imani hufanya kazi kama Nyota.Wakati wa Mchana Nyota huwa zinamulika/angaza lakini unaweza usizione.Ngoja giza liingie tu,utashangaa nyota zinavyo angaza kila upande angani.Vivyo hivyo imani ya mtu ndani ya Kristo Yesu.Wakati kupo kweupeee na hakuna matatizo imani inakuwepo ndani ya mtu lakini unaweza usijue kama huyu mtu anaimani kwa jinsi na kwa kiasi gani.Lakini wakati changamoto au matatizo yanapotokea ndipo utakapo ona jinsi gani imani ya mtu huyo inavyo mulika.

Ndio Maana nazipenda Changamoto Mtu wa Mungu maana zinaponijia,kwangu huona ni kama fursa ya kuidhihirisha imani niliyonayo ndani ya Kristo Yesu.Nasema nipetatizo,nipe changamoto,Nami nitakuonyesha imani Yangu!Shalooom!


"….mwenye haki ataishi kwa imani yake" (Habakuki 2:4)

No comments:

Post a Comment