Wednesday, June 27, 2012

“UNAJIFUNZA NINI KATIKA YALE ULIYOPITIA?” PART 1
Kila Hatua Ya Kimaisha Ambayo Mwanadamu Anapitia Ina Kitu Cha Kujifunza Ndani Yake.Haijalishi Ni Mbaya au Ni nzuri Kiasi Gani.Kama Utachukua Muda Wa Kuyatafakari Yale Uliyopitia Na Kuyageuza... Darasa La Kujifunzia Tena Kwa Mtazamo Sahihi, Basi Ni Dhahiri Utajifunza Mengi Na Yatakuimarisha Unapoelekea Kwenye Ubaadaye Wako(Hatima Yako).

Unapozigeuza Changamoto au Yale Uliyopitia Kuwa Darasa, Inakusaidia Kuchochea Na Kuimarisha Nguvu yako Ya Kusonga Mbele Na Ujasiri Wako Wa Kukabiliana Na Changamoto Mpya Utaimarika Kwa Namna Ya Kipekee.Kamwe Usije Ukapoteza Muda Wako Kulia,Kulalamika,Kujilaumu, au Kukata Tamaa,Huko Hakutaweza Kutakuletea Majibu Unayoyatafuta.Zaidi Hasa Kutazidi Kukudidimiza Na Kukukwamisha.Kamwe Usiangalie Umeshindwa Mara Ngapi,Angalia Umejifunza Mangapi Kwenye Yale Uliyoshindwa Kisha Chukua Hatua Usonge Mbele.Usikubali Kubaki Mahala Ulipodondokea na Kuendelea Kulia Au Kulalamika.Amua Kuinuka Huku Ukijitasmini Kwa Lengo La Kujifunza Kitu.Tamani Kujua Wapi Ulikosea,Kwanini Ulikosea, Na Lipi Ufanye Ili Usije Ukakosea Mara Ya Pili.

Hata Kama Ulifanya Vibaya Kiasi Gani,Ni Darasa Zuri Kwa Ajili Ya Kesho Yako.Ukijifunza Kwanini Ulikwama Kwenye Hilo Eneo,Na Kipi Ulipaswa Ufanye Ili Uvuke Hapo Mahala, Na Ukavielewa Vizuri.Ni Vigumu Sana Kukwama Tena Kwenye Eneo La Namna Kama Hiyo Endapo Litajatokea Kwa Mara Nyingine Baadaye.Ni Kwambie Ukweli Tu,Umekwama Na Husogei Kwasababu Hutakikujifunza Kwenye Hilo Lililo kukwamisha.
Hacha Kujilaumu, Hacha Kujichukia, Hacha Kuwalaumu Wengine.Kumbuka Wewe Si Wa Kwanza Kupitia Changamoto Kama Hizo.Wapo Waliopitia Changamoto Tena Yawezekana Za Kwao Ni Kubwa Kuliko Za Kwako Lakini Walivuka. Na Siri Iliyowasaidia Kuvuka Ni Pale Tu Walipoamua Kuzigeuza Changamoto Hizo Kuwa Darasa.

Badili Mtazamo Wako Juu Ya Yale Uliyopitia Na Uyafanye Kuwa Darasa Nami Naamini Utakayo Jifunza Yatafanyika Msaada Kwako Katika Kukupeleka Kwenye Kiwango Bora Zaidi.

"Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote ya kupendeza, yo yote yenye sifa njema, ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, YATAFAKARINI YAYO" <<Wafilipi 4:8>>

SAA YA WOKOVU NI SASA
MASSAWE GILBERT
bravothegreat@rocketmail.com

No comments:

Post a Comment