Sunday, July 29, 2012

“WEWE NI ORIGINO USIJARIBU KUISHI KAMA KOPI”

Umewahi Kufikiri Kwanini Tangu Misingi Ya Dunia Hii Ilipowekwa Mpaka Dakika Hii Unaposoma Post Hii ,na Hata Miaka Itakayokuja Huko Mbele,Hajawahi Kuwepo,Hayupo Na Hatakuwepo Mtu Mwenye Kufanana ...na Wewe Kwa 100%?

Kuzungumza Kwako, Kufikiri Kwako,Kutenda Kwako,Kuamua Kwako, Kwote ni Kwa Tofauti na Kwa kipekee Kabisa.Hata Alama Za Vidole Gumba Vyako Havifanani na Vya Mtu Yeyote Yule Hapa Duniani.Unadhani Ilitokea Tu Kama Bahati Mungu Aamue Kutumia Mda Wake,Ubunifu na Kila Alichotumia Ili Tu Akutengeneze Kwa Ustadi Mpaka Utoke Original Namna Hii? Ni Wazi Kabisa Mungu Angeweza Kuokoa Muda Wake Na Kuamua Kukufotokopi,Uzaliwe Kama Kopi Kutoka Kwa Wazazi Wako Lakini Hakufanya Hivyo,Akaamua Kukutoa Original Unafikiri Ni Bure Bure Tu?

Sikiliza Mtu Wa Mungu,Kamwe Usijaribu Kuishi Ishi Tu Ilimradi Siku Ziende,Tena Usijaribu Kuishi Kama Mtu Fulani Kwani Ni Hatari Kwa Habari Ya Hatima Yako.Mungu Ameamua Kukutengeneza Original Na Kuwekeza Vitu Hivi Vyote Vya Kipekee Ndani Yako Kwasababu Analo Kusudi La Kipekee Kwa Habari Ya Maisha Yako.Usijaribu Kuishi Kama Kopi,Mungu Haitaji Kopi Yako Anataka Origina Yako Maana Ndiyo Aliyoiandaa Kwa Ajili Ya Kutekeleza Makusudi Yake Hapa Chini Ya Jua.Shaloom!
See More

No comments:

Post a Comment