Saturday, May 12, 2012


"WEWE SI WA KAWAIDA, HUPASWI KUISHI KIKAWAIDA"


Kama ndani yako unatamani kufanya vitu visivyo vya kawaida tena ambavyo vinalenga kumpa Mungu utukufu, kamwe usikubali kuishi kama mtu wa kawaida.Ni lazima mfumo wako wa maisha ubadilike na usifanane na ule wa watu wanaoishi kikawaida kawaida.Ukitamani kufanya mambo ya siyo ya kawaida kamwe hawezi ukalala kwa jinsi ya kawaida, huwezi ukawaza kwa jinsi ya kawaida, hata kuamua kwako hakuwezi kuwa kwa kawaida kawaida.Maana ndani yako wewe si mtu wa kawaida hata kidogo tena umebeba vitu vya kimungu visivyo vya kawaida.


Watu wa kawaida kazi yao kubwa ni kungojea mambo ya tokee na kupokea,lakini watu wasio wa kawaida kazi yao kubwa ni kufanya mambo yatokee.Watu wa namna hii huona mahali ambapo wengine hawawezi kuona,huvuka mahali ambapo wengine hawawezi kuvuka,hufikiri mambo ambayo wengine wameshindwa kufikiria.Watu wasio wa kawaida hutafuta kwa bidii na kutoa majibu ya mambo mbalimbali ambayo yanaikabili jamii inayo wazunguka.

 Ni vema ukafahamu ya kwamba wewe si mtu wa kawaida na uko duniani kwasababu unahitajika na si kwa bahati mbaya hata kidogo. Mungu hajawahi na wala hatakuja kuumba kitu kisicho na kazi duniani. Najua unajua kuwa hata maua yana kazi na kama hivyo ndivyo je wewe si ni bora zaidi kuliko maua? Kumbuka yapo mambo yasiyo ya kawaida ambayo Mungu anataka kufanya kupitia wewe hapa duniani na hivyo kamwe usijaribu kuishi kama mtu wa kawaida.


 Wewe si wa kawaida na hivyo hupaswi ishi kimazoea.Mungu anategemea udhihirishe vile visivyo vya kawaida alivyoweka ndani yako ili ajipatie utukufu.Tena kumbuka usipofanya nafasi yako ujue kuna vitu havitakuja kufanyika na dunia itabaki kuwa na mapungufu kwa kutokufanya kwako sehemu yako.Ulivyopewa wewe ndani yako  si vya kawaida na hakuna mwingine aliyenavyo.Inuka uangaze maana wewe si wa kawaida!!!!!
Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu: maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. <<2 Petro 1:10>>

“Faith isn’t sitting around waiting for things to happen!” – Dani Johnson

No comments:

Post a Comment