Wednesday, June 27, 2012


UKITAKA MAFANIKIO ZIPENDE CHANGAMOTO
 Siku Zote Ni Vema Kumbuka Hili, “Maendeleo Yoyote Ni Matokeo Ya Changamoto Au Matatizo Yaliyotafutiwa Ufumbuzi”.Na Ndio Maana Kama Unapenda Maendeleo Au Unapenda Kusogea Hatua Nzuri Zaidi Katika Maisha Yako Ni lazima Uwe tayari Kuzipenda Changamoto. Ukizikimbia Changamoto Ujue Unayakimbia Maendeleo.

Hakuna Njia Mbadala, Ukitaka Kuyaendea Mafanikio, Mlango Mmoja wapo Utakaoupitia Ni Changamoto.Ukikabiliana Na Changamoto Kidogo Ujue Unatengeneza Maendeleo Kidogo,Ukikabiliana Na Changamoto Kubwa Au Nyingi Uwe Na Uhakika Ukishinda Itakupigisha Hatua Kubwa Kuliko Unavyodhani.

Ebu Kumbuka Jinsi Goliathi Alivyokuwa Ni Changamoto Kubwa Kwa Taifa La Israeli.Kila Mtu Akiwemo Mfalme Sauli Na Jeshi Lake Lote Walimwogopa Goliathi(Changamoto).Lakini Daudi Aliijua Siri Hii,‘‘Ukitaka Mafanikio Zipende Changamoto.” Alijua Hakukuwa Na Jinsi Yoyote Ya Yeye Kutoka Porini Kwenye Maisha Ya Kuchunga Kondoo Na Kwenda Kwenye Kiti Cha Ufalme(Kiwango Bora Zaidi) Bila Ya Kupambana Na Goliathi(Changamoto)

Goliathi Alikuwa Ngazi Ya Kumsaidia Daudi Avuke Kutoka Kwenye Uchungaji Kondoo Mpaka Kwenye Nafasi Ufalme.Hakukuwa Na Jinsi Nyingine Ilimlazimu Apambane Tu.Hakuna Njia Mbadala Mtu Wa Mungu Kama Unataka Kwenda Hatua Bora Zaidi Ya Kimaisha Ni Lazima Uzikabili Changamoto.Hata Yesu Ili mlazimu Aonje Mauti Ya Aibu Ili Akulete Wewe Na Mimi Kwenye Neema.Maandiko Yanasema,"Akiisha Kuziva Enzi Na Mamlaka, na Kuzifanya Kuwa Mkogo Kwa Ujasiri, Akizishangilia Katika Msalaba Huo" (Kol 2:15) .Umewahi Kufikiri Mtu Yuko Kwenye Mateso Lakini Anashangilia? Ndio Maana Kama Unakiu Ya Kutamani Mafakio Au Kutoka Mahali Ulipo Basi Ni Lazima Uwetayari Kuzishangilia Changamoto.

Mwamuzi wa Hatima ya Maisha yako Ya Leo Na Ya kesho ni wewe Mwenyewe na Si Mtu Mwingine.Ukiamua Kubaki Porini Kuchunga Kondoo Kwa Kuogopa Kukabiliana Na Goliathi Wa Kwako Wewe Ndie Muamuzi.Ukiamua Kujivika Ujasiri Na Kumkabili Goliathi Wako Wewe Ndiye Muamuzi. Chaguo Ni Lako Maisha Ni Yako. Kumbuka Hili Siku Zote, ‘‘Ukitaka Mafanikio Zipende Changamoto” Shaloom!

No comments:

Post a Comment